Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lake Oil yawasilisha pingamizi faini ya Bilioni 3.3 kwa Waziri Jafo

Lake Oil Pic Lake Oil yawasilisha mapingamizi faini ya Bilioni 3.3 kwa Waziri Jafo

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya uuzaji wa mafuta ya Lake Oil imewasilisha mapingamizi katika Wizara ya Muungano na Mazingira iliyo chini ya Waziri Selemani Jafo , kupinga adhabu ya kulipa faini ya shilingi bilioni 3.3 ya uchafuzi wa mazingira.

Itakumbukwa kuwa septemba 6 mwaka 2021, Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) iliwapiga faini kampuni hiyo yenye vituo vipatavyo 66 nchi nzima.

NEMC iliwapa siku 14 kumaliza adhabu hiyo , ambazo zimekwisha Septemba 21 mwaka 2021 huku ikiwa bado haijalipa faini hiyo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk.Samuel Gwamaka, amethibitisha kupokea mapingamizi yaliyowasilishwa na uongozi wa kampuni hiyo kufuatia adhabu waliyo pokea.

"Sheria ipo wazi na inasema kuwa kama NEMC haijakutendea haki katika maamuzi yoyote, basi unayo nafasi ya kuwasilisha mapingamizi kwa Waziri mwenye dhamana" Amesema Gwamaka.

Hata hivyo NEMC wamesema kuwa zipo kampuni nyingine za mafuta zaidi ya nane ambazo zinasubiri vibali maalum vya mazingira ambavyo vitawaruhusu kuanzisha vituo vingine zaidi vya mafuta nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live