Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Laini za simu milioni 35 zasajiliwa kwa alama za vidole nchini Tanzania

98923 Pic+laini Laini za simu milioni 35 zasajiliwa kwa alama za vidole nchini Tanzania

Fri, 13 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Laini za simu milioni 35.8 kati ya milioni 43 zimeshajiliwa kwa  alama za vidole  hadi  kufikia Machi 10, 2020.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Machi 13, 2020 na  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba katika maadhimisho ya  siku ya kimataifa ya haki  ya mteja.

Kilaba  amesema idadi  hiyo ni sawa na asilimia 83.1 ya  laini zote,  ni wazi kuwa zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole limekuwa na manufaa.

“TCRA iliasisi  mpango wa kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole mwaka 2018, zoezi hili limekuwa lenye manufaa  na kupata mwitiko mkubwa.”

“Hadi  kufikia Machi 10, 2020 idadi ya laini zilizounganishwa  mitandanoni ni 43,072,868 huku idadi ya laini zilizosajiliwa  kwa alama za vidole ni 35,813,455 sawa na asilimia 83.1 ya laini zote,” amesema Kilaba.

Amesema lengo la usajili wa kutumia mfumo huo ni kuimarisha usalama katika matumizi ya simu za mkononi , kulinda watumiaji na kufanikisha shughuli nyingine za usimamizi.

Pia Soma

Advertisement
Amebainisha kuwa wakati watumiaji wakiadhimisha siku ya mlaji ni muhimu wakakumbuka wajibu wa kila mmoja kusajili laini yake ya simu kwa mfumo wa bayometria kutumia kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa nchini(NIDA).

Akizungumzia kuhusu siku ya haki ya mteja,  Kilaba amesema siku hiyo huadhimishwa kila   Machi 15 na  maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiyu ya ‘Mteja Endelevu’.

“Kauli mbiu inajikita katika kusisitiza umuhimu wa upatikanaji wa huduma endelevu nasi katika sekta ya mawasiliano tumekuwa tukilitekeleza hilo, tunalitekeleza  na tutaendelea kulitekeleza wakati wote,” amesema.

Katika maadhimisho hayo TCRA imekuwa ikifanya mikutano mbalimbali na wadau kwa muda wa wiki  nzima  wakitoa elimu ya mawasiliano katika shule na vyuo mbalimbali katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Arusha, Zanzibar na Pwani.

Chanzo: mwananchi.co.tz