Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Laana ya Makonda yakwamisha makontena yake

17447 Makontena+pic TanzaniaWeb

Sun, 16 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Jumamosi Septemba 15, 2018 yameshindikana kuuzwa kwa mara ya nne mfululizo.

Makontena hayo yameshindikana kuuzwa katika mnada uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Soma zaidi:

:VIDEO: Makontena ya Makonda kaa la moto, yakosa mnunuzi kwa mara ya tatu

:TRA yakataa kuuza bidhaa mojamoja ndani ya makontena ya Makonda

Akizungumza kwenye mnada huo, mkurugenzi mtendaji  wa kampuni ya  udalali ya Yono, Scolastica Kevela amesema mnada huo umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana.

Kevela amesema hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazijafikia malengo waliyowekewa.

Soma zaidi.

:Mbunge ampongeza Waziri Mpango kwa kumshughulikia Makonda

:Msimamo wa Dk Mpango dhidi ya Makonda mjadala

“Ni kweli wateja wanakuja na bei lakini hazijafikia zile ambazo TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wametuwekea kama kodi yao," amesema.

Amesema wao kama madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.

Soma zaidi: Makontena ya Makonda, siasa za vinyonga nchini

Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo walionekana kutaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa.

Soma zaidi: Chadema yataka Makonda ajiuzulu

Chanzo: mwananchi.co.tz