Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LZ NICKEL LIMITED, Serikali zaingia mkataba wa mabilioni

6555bebb2166cfd61f183b965f59bb84 LZ NICKEL LIMITED, Serikali zaingia mkataba wa mabilioni

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Serikali ya Tanzania imeingia mkataba na Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED yenye mtaji wa thamani ya Dola za Marekani Milioni 664

Akizungumza leo, Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema serikali itanufaika na mapato ya mrabaha, kodi na tozo mbalimbali.

Makadirio ya awali kutokana na uzalishaji ni wastani Dola milioni 466 kwa mwaka.

Amesema serikali itakuwa na umiliki wa asilimia 16 za mradi zisizolipiwa wala kupungua thamani, hivyo kupata gawio kwenye faida baada ya kulipa kodi zote za serikali.

Profesa Kabudi amesema serikali itanufaika na tozo ya huduma, kodi ya mapato, zuio kwenye gawio na kodi nyingine zitakazolipwa na wafanyakazi na wakandarasi ambazo ni zaidi ya asilimia ya faida ya mradi.

“Fedha zote zitokanazo na mauzo zitahifadhiwa kwenye benki za ndani na hivyo kuimarisha uchumi,” amesema Kabudi

Aidha, waziri huyo amesema taarifa ya upembuzi ya mradi inaonyesha mradi huo utakuwa wa kipindi cha awali cha miaka 33 ya uzalishaji wa madini ya ‘nickel’ wa tani milioni 2.2 kwa mwaka.

Masharti:

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, Serikali iliipa masharti kampuni ya LZN likiwamo kwanza, ikamilishe bila kuhusisha serikali mazungumzo na Kabanga Nickel Company Limited ili kupata haki zote za kiolojia na mali zote ikiwemo nyumba na vifaa mbalimbali vya uchimbaj na utafiti.

Masharti mengine ni LZN kuingia mkataba na wanahisa hao ili kusiwepo madai yoyote dhidi ya serikali kuhusu eneo la Kabanga, LZN kujenga kiwanda cha uchenjuaji madini ya nickle na kuwa na uwezo wa kuchenjua madini mengine kama makinikia ya shaba na chuma kutoka Bulyahulu.

Profesa Kabudi aliyataja masharti mengine kuwa ni pamoja na kampuni ya LZN kukubali kuundwa kwa kampuni ya ubia kati yake na serikali na kwa pamoja itajihusisha na shuguli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini kupitia kampuni tanzu itakazosajili kwa madhumuni hayo.

“Pia, LZN ikubali kugawana faida za kiuchumi zitokanazo na uchimbaji, uchenjuaji na uuzaji wa madini hayo kwa usawa na haki bila kujali asilimia za hisa kwa mujibu wa sheria za Tanzania, pamoja na LZN kukubaliana na masharti ya serikali na kuanza majadiliano Oktoba, 2020 kiwanda kitajengwa Kahama mkoani Shinyanga,” alisema Kabudi.

Awali Profesa Kabudi alisema Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ambayo imefanyiwa mabadiliko makubwa na mabadiliko ya Sheria 2017 (Sheria Iliyoandikishwa na Mengineyo ya Mwaka 2017 (Written Law Miscellaneous Ammenfments 2017), ilifuta leseni 11 za wakala wa madini.

“Bila msimamo wako Mheshimiwa Rais (John Magufuli) thabiti, tungeyumba baada ya kubadilisha sheria watu walizoza, lakini nashukuru msimamo wako ulikuwa imara sasa manufaa yanaonekana” amesema Kabudi

Profesa Kabudi amefafanua akisema: “Mradi wa Kabanga ulianza muda mrefu. Mradi huu ulianza kufanyiwa utafiti mwaka 1976 hadi mwaka 1979 chini ya UNDP ukabaini kuwepo kwa madini ya nickel katika eneo la Kabanga, licha ya madini ya nickle, pia yapo madini ya shaba, dhahabu na platinum.”

Chanzo: habarileo.co.tz