Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LATRA yasitisha leseni za mabasi 22 nchini

Mabasi Md LATRA yasitisha leseni za mabasi 22 nchini

Tue, 21 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kuwa imesitisha leseni za usafirishaji abiria kwa mabasi 22 nchini Tanzania kuanzia Januari hadi February, 2023.

Johansen Kahatano ambaye nj Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara amesema hatua hi ni kutokana na vitendo vya kuingilia mfumo wa kufuatilia mwenendo wa magari (VTS) na kusababisha mfumo kutotuma taarifa ama kutuma taarifa kwa kurukaruka (skipping).

“Hapa kuna baadhi ya mabasi ambayo baada ya wataalamu wa Mamlaka kufanya chunguzi, waligundua betri za vifaa vya kufuatilia mwenendo wa mabasi (VTDs) zimeharibiwa na mfumo wa umeme kubadilishwa,” amesema Kahatano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live