Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusini yapangwa kimtindo sekta ya kilimo

Korosho Tandahimbaaa Kusini yapangwa kimtindo sekta ya kilimo

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan Septemba 20, 2023 alihitimisha ziara yake ya kimkakati ya siku saba katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani.

Yafuatayo ni mambo mbalimbali yaliyofanyika katika ziara yake kwenye sekta ya Kilimo.

Serikali kutekeleza mkakati wa kuingiza zao la Mbaazi na Ufuta katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (Warehouse Receipts System) ambao tayari umeimarisha bei ya Mbaazi kwa shilingi 2,300 kwa kilo; na kwa zao la ufuta kati ya shilingi 3,800 na 4,000 kwa kilo.

Rais Samia amezielekeza mamlaka husika kusimamia usafirishaji wa korosho ambapo sasa zitasafirishwa kwa meli badala ya magari na kutumika kwa vibali maalumu ikiwa msafirishaji atahitaji kutumia usafiri wa gari pamoja na kuruhusu bandari ya Mtwara kuanza usafirishaji wa zao hilo.

Serikali inaendelea na usajili wa mikorosho kwa mikoa ya Kusini pamoja na kutoa wito kwa Wakulima kuweka akiba ya fedha.

Rais Samia Suluhu Hassan amefungua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ghala la kuhifadhi nafaka za takribani tani 1,500 ambapo ghala hilo la mazao litasaidia kudhibiti sumu kuvu kwenye nafaka pamoja na kupima nafaka hizo ili kufahamu kiwango cha unyevu kilichopo katika nafaka hizo.

Wizara ya Kilimo kuja na mkakati wa kuongeza thamani ya zao la Korosho na Ufuta kupitia kuanzishwa kwa Kongani ya viwanda vya kuongeza thamani katika Korosho na Ufuta.

Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kongani hiyo eneo la Maranje, Nanyamba mkoani Mtwara pamoja na kuanzisha kiwanda cha cha kubangua korosho mkoani Lindi.

Serikali imeanza utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji maji ya mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani iliyowekwa kwenye mpango wa utekelezaji wa mwaka 2023/2024 ambao utawezesha umwagiliaji wa mashamba yenye hekta 49,307 kutoka hekta 13,270 za sasa kufuatia ujenzi wa mabwawa 21.

Aidha, jumla ya skimu 54 zenye ukubwa wa hekta 88,206 zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu kwa ajili ya kuanza utekelezaji.

Wizara ya Kilimo imejipanga kuwezesha wakulima kumudu uzalishaji wa mazao mengine ya nazi, ufuta na mbaazi kwa kugawa mbegu na miche bora na kutoa elimu ya kilimo bora cha mazao hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live