Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusajili ombi la kuchimba kisima Dar Sh60,000

28347 Kuchimba+pic TanzaniaWeb

Thu, 22 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bonde la Mto Wami/Ruvu limesema gharama ya kusajili ombi la kuchimba kisima jijini Dar es Salaam kwa matumizi ya nyumbani ni Sh60,000 na Sh150,000 kwa matumizi makubwa.

Taarifa ya Bonde hilo inaeleza kuwa ada ya mwaka kwa matumizi madogo ni Sh100,000 na matumizi makubwa Sh150,000.

Mbali na uchimbaji huo, taarifa hiyo inaeleza kuwa kwa wafugaji wa samaki, ombi la kuchimba kisima ni Sh60,000 huku ada yake kwa mwaka ikiwa Sh100,000 kwa matumizi madogo na Sh250,000 kwa matumizi makubwa.

Inaeleza kuwa kibali cha kuchimba kisima kwa ajili ya huduma za jamii kwa matumizi madogo ni Sh60,000 na matumizi makubwa ni Sh250,000. Ada kwa mwaka ni Sh150,000 kwa matumizi madogo na Sh250,000 kwa matumizi makubwa.

Inaeleza kuwa kibali cha kuchukua maji kwenye mto kwa ajili ya kilimo/umwagiliaji kwa matumizi madogo ni Sh150,000 na Sh250,000 kwa matumizi makubwa na ada kwa mwaka ikiwa Sh250,000 kwa matumizi makubwa.

Bonde hilo limebainisha kuwa vibali kwa ajili ya kuuza maji ni Sh250,000 kwa makundi yote madogo na makubwa huku ada zake kwa mwaka ikiwa Sh250,000 kwa matumizi makubwa.

Vibali kwa ajili ya matumizi ya nyumba za wageni kwa watumiaji wakubwa na wadogo ni Sh250,000 na ada ni Sh250,000 kwa matumizi madogo na Sh300,000 kwa matumizi makubwa.

Kwa viwandani, vibali vinatolewa kwa Sh250,000 kwa watumiaji wakubwa na wadogo na ada yake kwa mwaka kwa watumiaji wakubwa ni Sh300,000.

Vibali kwa wachimbaji madini wakubwa na wadogo ni Sh250,000 na ada yake kwa mwaka kwa watumiaji wakubwa ni Sh300,000.

Katika taarifa hiyo inaonyesha vibali kwa ajili ya nishati kwa watumiaji wakubwa na wadogo ni Sh250,000 na ada yake kwa matumizi makubwa ni Sh300,000.

 

 

 

 

 

 

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz