Bei za vyakula duniani zimeweka rekodi ya kupanda kwa mwezi Machi baada ya uvamizi wa Russia nchini Ukraine kutingisha masoko ya vyakula na mafuta ya kula, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema leo Ijumaa.
Kuvurugika kwa uuzaji nje kulikotokana na uvamizi wa Februari 24 na vikwazo dhidi ya Russia vimesababisha hofu ya tatizo la njaa duniani, hasa maeneo ya Mashariki ya Kati na Afrika, ambako athari zimeshaanza kuonekana.
Russia na Ukraine, ambazo maeneo yake makubwa ya kilimo cha nafaka ni kati sehemu zinazolisha dunia kw akiasi kikubwa, zinaoongoza kwa kuuza nje mazao kadhaa, yakiwemo ngano, mafuta ya kula na mahindi.
"Bei za vyakula duniani zilipanda kwa kiwango kikubwa mwezi Machi kufikia kiwango cha kuliko kuliko vyote vilivyowahi kufikiwa, wakati vita katika eneo hilo vikisambaza hofu katika masoko ya nafaka na mafuta," ilisema FAO katika taarifa yake.
Bei za vyakula za FAO, ambayo ilishatangaza kupaa kulikoweka rekodi mwezi Februari, zilipanda kwa asilimia 12.6 mwezi uliopita, "ikiwa ni ongezeko kubwa hadi kufikia viwango vipya vya juu kuliko vyote tangu vilipoanzishwa mwaka 1990", shirika hilo lilisema.
Viwango vya FAO, ambavyo hupimwa kwa kuangalia mabadiliko ya kila mwezi ya bei za vyakula kimataifa, vilikuwa na wastani wa pointi 159.3 mwezi Machi.
Kuchupa huko kw abei kunajumuisha rekodi ya bei ya mafuta ya kula, nafaka na nyama, FAO ilisema, ikiongeza kuwa bei za sukari na bidhaa za maziwa "pia zilipanda kwa kiwango kikubwa".
Russia imechangia asilimia 30 ya ngano na mahindi yote yanayouzwa duniani, wakati Ukraine ni asilimia 20 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, FAO imesema.