Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuondolewa kodi za simu janja, wauzaji shangwe

6886c61a7b2879853977dc64fc3b1236 Wauzaji simu kicheko, kuondolewa kodi kwenye simu janja

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKATI serikali ikisamehe kodi kwenye simu janga, vishikwambi na modemu, lengo likiwa kufikia asilimia 80 kutoka asilimia 46 iliyopo sasa ya watumiaji wa intaneti ifikapo 2025, Kampuni ya simu ya Oppo na Samsung wamesema kuondolewa kwa Kodi (VAT) kumeongeza wigo wa matumizi ya simu hizo kwa watanzania.

Bunge la Bajeti la mwaka 2021/22 limeondoa kodi ya asilimia 18 kwenye simu janja ili kila mwananchi aweze kutumia simu hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Usambazaji wa Bidhaa za kampuni ya Oppo, Mbwana Mpeta, amesema serikali imefanya jambo kubwa sana kwa kuondoa kodi katika simu janja ili kila mtanzania aweze kumiliki.

Amesema, wao kama kampuni ya Oppo wamejipanga kuweza kuhakikisha simu zao zinakuwa katika bei nafuu na kila mwananchi anapata fursa ya kumiliki simu janja na kuwa katika ulimwengu wa Kidijitali.

“Dunia imekuja ni kijiji, leo Oppo na Samsung tumezindua kwa pamoja duka hili katika jengo la China Plaza ukifika utapata simu aina zote na kwa bei nzuri lakini kikubwa ni kuondolewa kwa VAT hii inapelekea kwa sisi makampuni kupunguza bei za simu janja ili wananchi hadi wa kipato cha chini waweze kumiliki,”amesema

Naye Meneja Bidhaa wa Samsung, Julius Giabe amesema kwa sasa kuna soko kubwa la ushindani ila kwa upande wao wamejipanga kuleta bidhaa zenye ubora na uwezo mkubwa.

Ameishukuru serikali kwa kuondoa kodi (VAT) kwa simu janja na hiyo ni chachu ya kufanikisha Tanzania katika dunia ya kidijitali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live