Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kunambi ataka BBT ipitiwe upya

Kunambi Kunambiii.png Kunambi ataka BBT upitiwe upya

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi ametaka kupitiwa upya kwa mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), akitaja ujielekeze katika mkakati wa kuhakikisha vijana wanapata ajira.

Hoja yake hiyo inatokana na kile alichokifafanua, kwa kuwa mradi huo unahusisha hadi vijana waliohitimu elimu ya juu, hakuna atakayeendelea iwapo atapata fursa ya ajira katika taasisi yoyote hasa za fedha.

Kunambi ametoa hoja hiyo bungeni jijini Dodoma leo, Ijumaa Novemba 10, 2023 alipochangia mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2025.

“Hofu yangu ni kijana aliyemaliza chuo kikuu, umempa shamba la ekari tano, huku amefanya usaili Benki Kuu wamesema tunakuajiri, atabaki na hizo ekari tano aache ajira?” amehoji.

Ameeleza ni vema kupitia upya mradi huo, pamoja na nia njema iliyopo, lakini ni muhimu kuangalia mkakati wa utekelezaji ili vijana wapate ajira.

Katika mchango wake huo, Kunambi pia alipendekeza kuanzishwe utaratibu wa halmashauri kufikia hatua ya kujitegemea, badala ya kutegemea Serikali Kuu wakati wote.

“Ni muhimu tufikiri tofauti, halmashauri zote zianze kuwekeza, zianze kufikiria kujitegemea, sisi Mlimba tunajenga vituo vya afya vitatu kwa mapato ya ndani, hakuna sababu za kufanya halmashauri isijitegemee,” amesema.

Mbali na Kunambi mwingine aliyechangia kuhusu mpango huo ni mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima akipendekeza maofisa ugani wahamishwe kutoka kusimamiwa na halmashauri na wawe chini ya tume ya umwagiliaji.

Amesema kufanya hivyo kutaongeza usimamizi wa watumishi hao na hatimaye ufanisi katika utendani kuimarika.

Hoja nyingine iliyotolewa naye, ni mpango huo ujikite katika utafiti wa kilimo na maendeleo zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live