Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna muda unatamani kwenda kwa mganga kisa faini - Mfanyabiashara

Dsf Mwajombe Kuna muda unatamani kwenda kwa mganga kisa faini - Mfanyabiashara

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Onesmo Mwajombe mfanyabiashara wa mjini Njombe amesema nchi yoyote ambayo imekuwa ikitoa faini zisizoeleweka kwa wananchi wake na hushindwa kuendelea kutokana na manung'uniko ya wananchi yanayozalisha laana.

Ameeleza hayo katika kikao cha Jumuiya ya wafanyabiashara mkoani Njombe mbele ya viongozi wa Jumuiya hiyo taifa walipokuwa wakizungumza na wafanyabiashara kwa lengo la kujua kero,changamoto na hali zao.

"Nchi yeyote inayotegemea kutoa faini za ajabu ajabu ni kama inakuwa na laana kwasababu watu wananung'unika hatutoi kwa raha, tuko tayari hata kwenda kwa waganga na kumweleza mganga wa kienyeji tusaidiane kwasababu hii faini! yaani tunaingia mpaka kwenye dhambi kutokana na sheria zilizotungwa," amesema Mwajombe.

Hamis Livambe ni mwenyekiti wa Jumuia ya wafanyabiashara Tanzania amekiri uwepo wa faini ambazo wamekuwa wakitozwa wafanyabiashara ambazo zimegawanyika katika pande mbili huku lengo la faini hizo ikiwa ni kurekebisha tabia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live