Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumekucha Dar Awamu ya Pili Ujenzi DMDP

Kariakoo Pic 780x470 Kumekucha Dar Awamu ya Pili Ujenzi DMDP

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imeanza maandalizi ya kuanza Awamu ya Pili ya Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(DMDP), ili kuanza utekelezaji wa ukarabati wa barabara kongwe ambazo nyingi zinahitaji kujengwa upya.

Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura), Mkoa wa DSM,Geofrey Mkinga amesema maandalizi ya awali ya kumpata mkandarasi yameshaanza ili utekelezaji wa mradi huo uanze.

“Kuanzia sasa hivi kuna wahandisi washauri wanafanya usanifu kwenye hizo barabara zetu kuhakikisha tunapata mahitaji halisi na ubora ule na kujua gharama ikifika Novemba tutatangaza zabuni na mwezi wa tatu wanne watano tutakuwa na wakandarasi kupitia mradi huo DMDP,”amesema Mkinga.

Hatahivyo amesema ukarabati mdogo wa barabara za mjini kati, unatarajia kuanza Septemba mwaka huu endapo ataweza kupatikana mkandarasi.

“Sisi kupitia hela za matengenezo ya kawaida kama tulivyofanya katika barabara ya Jamhuri tunaziba mashimo kuna baadhi ya maeneo tutaweka lami nyingine juu yake, kwa sababu lami iliyoko pale baada ya kuziangalia lile tabaka la udongo chini halijaharibika sana ni hili tabaka la juu tutaziba mashimo .

“Haya maeneo mengine tutafanya ovaring kuweka lami ya juu yake, ili isiharibike lakini yale mengine tutayaziba haya tunayafanya lini hayo tunafanya mwezi huu wa tisa sasa hivi tunawatafuta wakandarasi,” amesema Mkinga.

Mkinga amefafanya kuwa awali mtandao wa barabara zaidi ya kilomita 25,000 haukuwa mzuri, ambapo asilimia 57 za barabara hizo zilikuwa katika hali mbaya, jambo ambalo lilimfanya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuongeza fedha, ili baadhi ya barabara hizo zikarabatiwe.

“Kuna asilimia 11 zina hali nzuri mtandao wa barabara, lakini asilimia 39 yenyewe kuna hali ya wastani, kwa hiyo sasa fedha za matengenezo tunatengeneza wapi, fedha za matengenezo tunatengeneza barabara zina hali nzuri na wastani ili zisiende kwanye barabara zenye hali mbaya,” alisema Mkinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live