Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuhusu mradi bomba la mafuta...

EACOP Bombaaaa Mafuta.jpeg Kuhusu mradi bomba la mafuta...

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima - Uganda hadi Chongoleani - Tanga unaendelea kushika kasi, baada ya kukamilika kwa hatua za ujenzi wa vituo vya kupokea mabomba.

Mratibu wa mradi huo Asiad Mrutu amesema katika kituo namba saba kwenye kijiji cha Mkongo wilayani Chato mkoani Geita kazi inaendelea kwa kasi, ili kuikamilisha na kuanza kupokea mabomba yatakayokuwa yakizalishwa Sojo wilayani Nzega mkoa wa Tabora.

Mrutu amesema Serikali imeendelea na usimamizi madhubuti wa mradi huo huku akiwapongeza Watanzania kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye mradi huo.

Kati ya Wafanyakazi 225 waliopo katika kituo hicho, Watanzania ni 223.

Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki lenye urefu wa kilomita 1,447 utagharimu shilingi Trilioni 11 hadi kukamilika kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live