Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuhifadhi makasha ni bure bandari ya Mtwara

Bandari Mtwaratt Kuhifadhi makasha ni bure bandari ya Mtwara

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeondoa tozo ya kuhifadhi makasha kwenye Bandari ya Mtwara kwa watumiaji wa bandari hiyo katika msimu huu wa korosho.

TPA pia imepunguza kwa asilimia 30 gharama za kupakia na kupakua shehena ya makasha yenye mizigo yanayoingia na kutoka bandarini pamoja punguzo la gharama kwa 0.5% ya matumizi ya gati kwa shehena za makasha zinazoingia na kutoka katika bandari hiyo.

Mbali na kupunguza gharama hizo, TPA imeongeza muda wa kuhifadhi makasha yenye shehena kutoka siku saba hadi 14 bila malipo.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dkt. Geogre Fasha amesema lengo la kupunguza gharama hizo ni kuwawezesha watumiaji wa Bandari ya Mtwara kupata unafuu wa kusafirisha na kupakua shehena kupitia bandari hiyo.

"Bandari ya Mtwara kwa sasa imepewa dhamana kubwa ya kuwa kiungo pekee cha kusafirisha korosho zote za mikoa ya Kusini mwa Tanzania kwenda nje ya nchi kulingana na mahitaji ya wateja na wadau wa zao hilo hivyo na sisi tumeona tuwapunguzie gharama na tozo mbalimbali ili iwe rahisi kwa wateja wetu kusafirisha shehena zao," amesema Dkt. Fasha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live