Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kufutwa tozo kutachochea biashara

Tozo Pc Data Kufutwa tozo kutachochea biashara

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, wamesema kuwa kufutwa kwa tozo mbalimbali kulikofanywa na serikali hivi karibuni kutakuwa kichecheo kikubwa cha kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kupanua biashara kati yao na Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) sambamba na kuzuia magendo.

Wananchi hao wamesema hayo mbele ya mbunge wa jimbo la Buhigwe, Felix Kavejuru alipokuwa akifanya mikutano ya hadhara kwenye vijiji vya Kibwigwa na Mkatanga kwenye jimbo hilo, akiwa kwenye ziara ya kutembelea jimbo na kueleza miradi inayotekelezwa na serikali.

Mmoja wa wananchi hao, Justin Wilson alisema kuwa baada ya amani kurejea nchini Burundi, kumekuwa na fursa kubwa ya kufanya biashara na nchi hiyo, lakini kulikuwa na changamoto kubwa ya tozo nyingi ambazo zilikuwa kero na kuwakatisha tamaa wajasiRiamali wengi kushindwa kufanya biashara za kuvuka mpaka.

Kwa upande wake Tumaini Razalo aMRsema kuwa uwepo wa tozo nyingi kwenye shughuli za biashara, ilikuwa changamoto kubwa kwa wafanyabiashara na kuwalazimu wengi wao kupita njia za panya na hivyo kuinyima serikali mapato.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara kwenye vijiji hivyo, Kavejuru ameema kuwa serikali imepunguza tozo kwenye biashara mbalimbali kutoka tozo 380 zilizokuwepo hadi kufikia tozo 144, lengo likiwa kutoa unafuu wa kodi kwa wafanyabiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live