Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuchelewa hati ya kusafiria EAC kwakwamisha biashara

D12eaec2f8dd1ff5a96e27ccdc43788b Kuchelewa hati ya kusafiria EAC kwakwamisha biashara

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo cha washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kushindwa kupitisha haraka hati ya kusafiria ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACpass), kinatatiza biashara ya mipaka katika ukanda huo.

Kushindwa kuanza kutumika hati hiyo kumechangiwa na ukosefu wa uratibu wa nchi sita wanachama kwenye majaribio ili kurahisisha uvukaji mipaka kwa wananchi wan chi wanachama wa jumuiya hiyo.

Hayo yalibainishwa kwenye Kongamano la Kuwezesha Biashara la Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) kuhusu biashara katika mpaka wa Holili wiki iliyopita.

Madereva wa malori pamoja na wafanyabiashara wadogo walionyesha wasiwasi wao juu ya taratibu zisizoratibiwa za uidhinishaji wa bidhaa na watu, hasa kuhusiana na vizuizi vya Covid-19.

Wafanyabiashara wadogo walilalamika kuwa wakati vipimo vya Covid-19 vilikuwa bure katika nchi moja, walilazimika kulipa Dola za Marekani 10 kwa vipimo vya antijeni katika nchi nyingine.

Mkutano wa mawaziri wa afya wa kikanda uliofanyika Desemba, mwaka jana uliidhinisha hati hizo kama jukwaa la kikanda la kuwezesha wasafiri wote katika kanda hiyo na kwingineko.

Mwezi uliopita, EABC ilitoa angalizo kupitishwa kwa hati hiyo ya kusafiria ya kidijitali ba cheti cha Covid-19 vinavyokubaliwa na EAC.

Hatua hiyo pia ilichukuliwa kama sehemu ya kuondoa vikwazo vya biashara ambavyo vitahakikisha ufufuaji wa haraka na uthabiti wa uchumi wa EAC kutokana na athari za Covid-19.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya EAC wa Kenya, Kevit Desai alisema hatua zisizokubaliana kuhusu Covid-19 zimeongeza gharama ya uendeshaji wa biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, John Kalisa alisisitiza kuwa ipo haja ya kuanzishwa kwa haraka kwa EACPass ili kuwezesha kuongezeka kwa biashara katika kivuko cha mpaka cha Holili/Taveta.

Sekretarieti ya EAC inasisitiza kwamba kuoanishwa kwa gharama za Covid-19 na muda ulioratibiwa wa kungojea matokeo ya Covid ilikuwa muhimu ili kuwezesha kuendelea kwa biashara na kupunguza muda katika maeneo ya mpaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live