Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Korosho za Ruvuma, Mtwara na Lindi zitumie bandari ya Mtwara

Majaliwa Lindi Ed Korosho za Ruvuma, Mtwara na Lindi zitumie bandari ya Mtwara

Sun, 6 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Taarifa hiyo imewasilishwa leo Juni 6, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipokuwa katika kikao na wadau wa zao la korosho kulichofanyika katika ukumbi wa hoteli wa Sea View mjini Lindi.

Amesema Rais Samia amewaagiza viongozi wa bandari wapitie tozo zote zinazowakwaza wasafirishaji ili kuwavutia kuitumia bandari hiyo "tunataka wasafirishaji watumie bandari hii kusafirisha korosho kuanzia na msimu huu".

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa wakulima wakubali kupokea pembejeo kulingana na mahitaji yao na watalipia kulingana na idadi ya mifuko waliyochukua na sio shilingi 110 kwa kila kilo kama inavyelezwa “kila kilo ni gharama mno, lengo letu ni kuendelea kumpungumzia mzigo mkulima, msiogope kuchukua pembejeo”

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wadau wote wa korosho nchini katika kufanikisha mkakati huo ikiwemo kutengeneza mashine za ubanguaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO)

"Ni vyema tujikite kwenye ubanguaji kuliko kuisafirisha nje ya nchi ikiwa ghafi, tumeandaa mfumo mzuri na Rais wetu ameendelea kusisitiza katika ujenzi wa viwanda"

"tusisikie makato ya unyaufu kwasababu yanawafanya wanunuzi wahisikuwa wanaonewa, viongozi wa Serikali tusimamie hilo, hatutaki kusikia kuhusu tozo ya unyaufu" amesema Waziri Mkuu.

Chanzo: ippmedia.com