Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Korosho kuanza kuuzwa Septemba Mosi

Aab951b7d689409215a3d52332d98a30 Korosho kuanza kuuzwa Septemba Mosi

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametangaza kuwa msimu wa mauzo ya korosho ghafi kwa mwaka 2020 na 2021 unatarajiwa kuanza Septemba Mosi mwaka huu

Amesema, makadirio ya msimu wa uzalishaji kwa mwaka 2020/2021 yanatarajiwa kuongezeka kutoka tani 232,000 za msimu 2019/2020 hadi tani 300,000

Hasunga aliwaeleza hayo waandishi wa habari mkoani Lindi kuwa, baada ya kufungua mkutano mkuu wa wadau wa korosho.

Alisema, Serikali imetambua umuhimu wa kutumia fursa ya kijografia kwa kuwa Tanzania inapoingia kwenye msimu wa mauzo ya korosho nchi nyingi bado zinakuwa hazijaanza mavuno.

Hasunga alisema, kiwango cha uzalishaji kinatarajiwa kufikiwa endapo hali ya hewa itaruhusu, matumizi sahihi ya viuatilifu na usimamizi thabiti wa mauzo ya korosho za wakulima kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Alisema, Bodi ya Korosho kwa kushirikiana na wadau imeandaa taratibu za usimamizi wa masoko na mauzo ya korosho ghafi na kwamba kila mdau amepewa majukumu katika usimamizi.

Aidha, taratibu zote na mgawanyo wa majukumu umezingatia maelekezo na maazimio ya wadau kupitia Mkutano Mkuu wa mwaka huu uliofanyika juzi mkoani Lindi.

Hasunga alisisitiza kuwa minada ya mauzo ya korosho itaanza mara tu baada ya korosho ghafi kuingia katika maghala ya minada na wanunuzi kukamilisha taratibu za kupata leseni ya ununuzi kutoka Bodi ya Korosho Tanzania.

"Ni imani yangu kuwa kila mdau tayari amekamilisha maandalizi ya msimu kabla ya ununuzi kuanza" alisema.

Aliwataja wadau hao kuwa ni pamoja na; sekretarieti za mikoa, halmashauri za wilaya, wakulima, vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, waendesha maghala, wasafirishaji, wanunuzi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), na wengine wanaohusika kwa namna moja au nyingine katika .

Chanzo: habarileo.co.tz