WAKUU wa Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma wamekubaliana kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan lililoamuru kusafirisha mazao ya korosho nje ya nchi kupitia bandari ya Mtwara.
Katika tamko la pamoja wamesema sasa ni rasmi korosho zote zinazozalishwa katika Mikoa hiyo zitasafirishwa kupitia bandari hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa masoko ya korosho msimu wa mwaka 2023/2024 kilichofanyika mkoani Mtwara.
Amesema wamekaa kwa pamoja kujadili namna ya kutekeleza agizo hilo na kwa pamoja wamekubaliana kufanya utekelezaji kwa kusimamia maagizo hayo ipasavyo na kuwataka wadau wote kutekeleza makubaliano hayo.