Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kongamano uchumi wa buluu kufanyika DSM

Uchumi Wa Buluu Kongamano uchumi wa buluu kufanyika DSM

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Regional Maritime cha Ghana, vitafanya kongamano la tatu la kimataifa la uchumi wa buluu nchini Tanzania mwezi Julai katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Julius Nyerere (JNICC).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 15, 2024, Mkuu wa wa Chuo cha DMI, Dkt. Tumaini Gurumo amesema lengo la kongamano hilo ni kukutanisha wadau wa uchumi wa buluu kujadiliana na kubadilishana uzoefu ili kukuza uchumi wa buluu.

Amesema kongamano hilo litakuwa na kaulimbiu itakayohusisha mambo matatu; ulinzi na usalama baharini, mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo ya teknolojia katika uchumi wa buluu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live