Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kondoa kuzalisha tani 100,000 za alizeti

Wakulima Alzeti Kondoa kuzalisha tani 100,000 za alizeti

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma inatarajia kuzalisha tani 100,000 za alizeti kwa msimu wa masika wa mwaka 2022 ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Hamisi Mkanachi wakati akizungumza kwenye mafunzo ya vitendo kwa wakulima na maofisa ugani kwenye mashamba darasa wilayani humo.

“Sisi tumejiwekea mkakati wa kuzalisha tani 100,000 na katika kuthibitisha hilo kwenye shule zetu za msingi, sekondari, vyuo na maafisa ugani wote waliopata mafunzo wanalima alizeti” amesema

Mkanachi amesema Kondoa imepata tani 11 za mbegu bora za alizeti na tayari wameuza tani 4.7 hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia tani 6.3 zilizobaki ambazo wilaya imewafikishia kwenye maeneo yao.

Amesema wilaya imegwawa kilo 6 za mbegu za alizeti kwa kila ofisa ugani na Halmashauri imelima ekari 60 za alizeti ikiwa ni kuonyesha mfano kwa wananchi wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Nyasebwa Chimangu amewataka maofisa ugani na wakulima kutumia fursa za mvua inayoendelea kunyesha kuzalisha kwa wingi zao hilo ambalo hustawi zaidi kwenye ardhi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live