Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kodi kwenye mabasi makubwa yashushwa

Bus Bus Bus Kodi kwenye mabasi makubwa yashushwa

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imependekeza kushushwa kwa kodi ya mapato kwa wasafirishaji wa abiria na mizigo kwa kutumia viwango elekezi vya kodi kwa kila gari kutoka Sh milioni 2.7 kwa luxury na Sh milioni 2.4 kwa basi la kawaida hadi Sh milioni 2.2

“Napendekeza kurekebisha Kifungu cha 65T cha Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332, kwa kuweka utaratibu wa kukadiria kodi ya mapato kwa wasafirishaji wa abiria na mizigo kwa kutumia viwango elekezi vya kodi kwa kila gari.

“Utaratibu huu utahusisha walipakodi binafsi (Individuals) pekee ambao hawana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha ritani za kodi. Lengo la hatua hii ni kutatua changamoto za utekelezaji wa utaratibu uliopitishwa hapo awali wa kuwataka walipakodi wanaoandaa na wasioandaa hesabu za kodi kulipa kodi za awali kulingana na viwango elekezi vya kodi kwa kila gari.

“Viwango elekezi vya kodi vinavyopendekezwa sasa vitatumika kwa walipakodi binafsi pekee ambao mauzo ghafi yao hayazidi kiasi cha Sh milioni 100 na ambao hawawajibiki kuandaa hesabu kisheria. Aidha, maboresho ya viwango vya kodi elekezi kwa kila gari yanalenga kutoa unafuu wa kodi kwa kundi husika na hivyo, kurahisisha utekelezaji wa takwa la kisheria,” Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live