Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kodi biashara za mitandao mjadala mwingine

Mtandao Biashara Kodi biashara za mitandao mjadala mwingine

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjadala umeibuka kuhusu hatua ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutaka biashara za mtandaoni kulipiwa kodi.

Juzi Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira katika ukurasa wake wa Twiter, aliandika akihoji sababu ya biashara za mtandao kutotozwa kodi.

“Biashara ikifika mauzo ya Sh4 milioni TRA wanatoza kodi na biashara inapofikia mauzo ya 100 milioni wanasajili kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kutozwa kodi kulingana na faida, Kwa nini biashara za mtandao zisitozwe kodi hata zikifikia mauzo stahiki?” aliandika.

Kufuatia mjadala huo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifafanua kuwa kila mtu anayefanya biashara ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zikiwemo za mitandao anapaswa kulipa kodi.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema biashara yoyote inayofanywa na mauzo yake kufika Sh4 milioni, mfanyabiashara anapaswa kulipa kodi.

“Sheria iko wazi na imeeleza mtu anayefanya biashara ndani ya siku 15, anapaswa awe amejisajili ni biashara gani anafanya na ni wapi anapofanyia,” alisema Kayombo.

Kuhusiana na kituo cha malipo, Kayombo alisema biashara ya kwenye mitandao ni biashara kama biashara nyingine na utaratibu wa malipo ni ule ule haubadiliki.

Hata hivyo, Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile alipingana na kauli hiyo kwa kuandika kwenye mtandao wake wa twitter: “Tanzania bado tuko nyuma sana katika biashara ya mtandao, tunahitaji kuikuza na kuilea, vijana wengi wamejiajiri kupitia mfumo huu.

“Kwanza kutoza kodi mapema kutadumaza mfumo huu na kuna biashara nyingi, nguvu ielekezwe katika kuimarisha usalama na imani.’’

Wasemavyo wafanyabiashara

“Kuna kitu watu wengi hawajakifahamu, tunaofanya biashara wengi kwa njia ya mtandao tuna maduka na tunalipa kodi zote, labda angefafanua zaidi ni watu gani wanalengwa,” alisema mfanyabiasha wa viatu, Flaviana Temba.

Mfanyabiashara wa nguo, Aisha Mustapher alisema: “Kuna wale wenye maduka wanalipa kodi na wapo wasio na maduka, unakuta mtu anahifadhi bidhaa ndani au anatembea nazo kwenye gari, wengi wao ndio wasiolipa kodi”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCRA, Dk Jabiri Bakari alisema jukumu la mamlaka hiyo ni kuwasimamia wanaotoa huduma za mawasiliano (maudhui) na sio kuwasimamia wanaotangaza matangazo yao ya biashara.

“Sisi tunasimamia watoa huduma za mawasiliano kisekta, hayo matangazo au biashara ya bidhaa wanayoweka haituhusu, badala yake inawahusu watu wa TRA,” alisema Dk Bakari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live