Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizungumkuti bei bidhaa za chakula

Bei Za Bidhaa 4.crdownload Kizungumkuti bei bidhaa za chakula

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bidhaa za nafaka jijini Tanga zimepanda bei zikiongozwa na unga wa ngano ambao umepanda kutoka Sh 1,300 hadi Sh 2,000 kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu.

Ambapo bei katika bidhaa za viwandani zikiwamo mafuta, sukari na sabuni ambapo sukari imepanda kutoka Sh2,000 hadi Sh2,800.

Bidhaa nyingine zilizopanda kwa kipindi cha Januari hadi Machi ni mchele kutoka Sh1,500 hadi 2,200 kwa kilo moja, maharage 1,800 hadi 2,200, unga wa sembe kutoka 1,800 hadi Sh2,000 na viazi mviringo kutoka Sh800 hadi Sh1,000.

wenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Soko la Ngamiani jijini humo, Jafari Mungereza amesema unga wa ngano umepanda bei kwa kasi, jambo linalowashangaza kwani ni bidhaa ambayo huwa haipandi bei kabisa sokoni.

“Bidhaa nyingi za vyakula zimepanda bei kiasi kikubwa, tunaiomba Serikali iingilie kati ili kuwanusuru wananchi wa kipato cha chini kwani ndiyo waathirika wakubwa na mfumuko huo wa bei,” amesema.

Kwa upande wa bidhaa za viwandani zikiwemo sabuni na mafuta ya kupikia, mfanyabiasha bidhaa hizo, Mohamed Suleiman amesema sabuni za mche zimepanda kutoka Sh2,000 hadi Sh3,000 na mafuta ya kupikia ya lita 20 kwa sasa ni Sh 111,000 kutoka Sh 60,000 ya zamani.

Naye mfanyabiashara wa mboga na matunda sokoni hapo, Miraji Saidi amesema bidhaa hizo zinapanda kutokana na mazao hayo kutegemea mvua.

“Bidhaa za matunda na mboga mboga mara nyingi hutegemea mvua na hadi sasa mvua hazijanyesha kwa muda mrefu kumekuwa na ukame, hivyo tunaiomba Serikali isimamie utunzaji wa mazingira ili mvua tuweze kupata mvua za asili," amesema.

Naye Ofisa Biashara wa halmashauri ya jiji la Tanga, Lucia Marandu amekiri kuwepo kwa ongezeko la bei katika bidhaa mbalimbali na kuongeza kuwa suala hilo siyo kwa mkoa na Tanga pekee bali na mikoa mingine, ameomba muda zaidi ili afuatilie sababu zinasobabisha mfumuko wa bei.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live