Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda chadaiwa kuzalisha mafuta ya kula machafu

Machafuu Kiwanda chazalisha mafuta ya kula machafu

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: eatv.tv

Ili kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia nchini kumepeleka baadhi ya wafanyabishara wasio waaminifu jijini Mwanza kuzalisha mafuta katika mazingira machafu na kuwauzia wananchi.

Submitted by Agnes Kibona on Ijumaa , 22nd Jul , 2022 Baadhi ya ndoo zinazohifadhia mafuta machafu

Tumefika katika eneo la Igogo wilayani Nyamagana, katika kiwanda cha Voil ambacho mamlaka husika zilisitisha uzalishaji wa mafuta katika kiwanda hicho miaka mingi iliyopita kutokana na changamoto ya uendeshaji wake lakini leo hii kinazalisha mafuta kinyemela katika mazingira hatarishi.

Aidha, wananchi wakazi wa eneo hilo ambao ndiyo watumiaji wa mafuta hayo wamelaani uzalishaji wa mafuta hayo kuendelea na kusema wengi wanaugua magonjwa ya moyo kutokana na kutumia mafuta mabaya ambayo hajathibitishwa.

Dickson ni mtendaji wa Kata ya Igogo na Ramadhan Mahela ni diwani wa Kata hiyo, wamesema wanafahamu kuhusu kiwanda hicho kutengeneza mafuta machafu huku wakitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatua.

Chanzo: eatv.tv