Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha mifuko ya plastiki chanaswa Boko

Matumizi Ya Mifuko Ya Plastiki 660x400.jpeg Kiwanda cha mifuko ya plastiki chanaswa Boko

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akiwa ameambatana na na Timu yake wamefanikisha kukamatwa kwa shehena ya mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku na Serikali kutumika nchini kutokana na kuharibu mazingira.

Mifuko hiyo imekamatwa ikiwa inatengenezwa kwenye kiwanda kinachomilikiwa na Raia wa Kichina kiitwacho Toco & Company Limited kilichopo eneo la Mbezi Juu Kata ya Wazo Jijini Dar es salaam ambapo ameagiza kiwanda hicho kifungwe na Mamlaka husika wakiwemo NEMC, TBS, TRA na Polisi wachukue hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria.

DC Mtambule amesema kuwa mifuko hiyo inayochafua mazingira inauzwa Wilaya zote za Dar es salaam na tayari ameongea na Ma-DC wenzake ili washirikiane kuwakamata wote wanaoitengeneza, kusambaza na kuitumia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live