Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na rais na mtendaji nwa kampuni ya Elsewedy Electric kutoka nchini Misri, Mhandisi Ahmed El Sewedy, leo Agosti 13,2021 , Ikulu Chamwino Dododma.
Katika mazungumzo yao Mhandisi huyo amethibitisha kuwa tayari wamesha jenga kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme , transfoma, mita za umeme , katika eneo la kigamboni jijini dar es salaam, kitakachofunguliwa mwezi desemba 2021.
Ameongeza kusema kuwa kutokana na ushirikiano mzuri walioupata kutoka kwa Serikali, wanatarajia kufungua viwanda vingine zaidi kama cha mbolea na kuwekeza katika ujenzi wa Reli mpya ya kisasa ili kuunga mkono juhudi za Serikali.
Rais Samia, amemshukuru Muhandisi huyo na kumuhakikishia kuwa serikali itampa ushirikiano wa kutosha ili kutekeleza miradi hiyo kwa muda muafaka