Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha kutengeneza betri za magari chazinduliwa mkoani Pwani

73204 Kiwandapic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rufiji. Mkuu wa Mkoa wa Pwani nchini Tanzania, Everist Ndikilo amewataka wananchi kushirikiana na wawekezaji ili kuwa mabalozi wa kuvutia uwekezaji nchini.

Ndikilo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 27, 2019 katika uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata betri za magari zilizotumika cha Huatan Investment kilichopo kijiji cha Nyamwange Wilaya ya Rufiji.

"Tukiwapa ushirikiano wawekezaji wetu wataleta wengine. Tuwe na matumizi bora ya ardhi, mkulima akae eneo lake na mfugaji akae eneo lake.”

“Maeneo ya wawekezaji nayo tuyaache wakija kuwekeza msiwauzie kwa bei ya kuwaumiza iwe ina manufaa kwa pande zote," amesema.

Amebainisha kuwa kuna wawekezaji kutoka Uarabuni wanataka kuwekeza katika kiwanda cha sukari kitakachotoa ajira kwa watu wengi zaidi.

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) kanda ya Mashariki,   Venance Mashiba amesema uwekezaji huo ulipitia katika kituo hicho mwaka 2017 na gharama ya uwezeshaji ilitajwa kuwa ni Dola 630,000  za Marekani sawa na Sh1.5 bilioni.

Pia Soma

Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Xian Ding amesema kiwanda hicho kinachakata betri zilizotumika tani 10,000,  kitatoa ajira za moja kwa moja 60 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 200.

"Kwa kuanza tutakuwa tukisafirisha malighafi kwenda nje ya nchi zinazotokana na betri zilizochakatwa kwa ajili ya kutengeneza betri mpya.”

“Lakini baada ya mwaka mmoja mpaka miwili ijayo kulingana na ustawi wa biashara tutaanza kuwa tunachakata na kutengeneza betri Tanzania kwa ajili ya soko la ndani," amesema Ding.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz