Menu ›
Biashara
Fri, 6 May 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mtendaji wa Kampuni hiyo ambayo iliingia mkataba wa kufungasha, kuuza na kusambaza chanjo ya Johnson & Johnson Barani Afrika amesema kuwa Kampuni hiyo ipo mbioni kufunga kwa kuwa hawajapokea oda yoyote kwa kipindi kirefu.
Shirika la Afya ya Umma-Afrika limewataka wanaonunua Chanjo ya COVID 19 Barani humo kuagiza katika Kampuni ya Aspen Pharmacare ya Afrika Kusini, likisema soko ni muhimu katika kuendeleza utengenezaji wa chanjo katika Bara hilo.
Aidha, Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kilisema kinafanya kila linaloweza nyuma ya pazia kuzuia Aspen kufunga kituo chake.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live