Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha chai kuanza Septemba

Chai Ed Kiwanda cha chai kuanza Septemba

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiwanda cha Chai cha Mponde kinatarajiwa kuanza uzalishaji wake Septemba mwaka huu, 2022 baada ya serikali kuingilia kati na kukifufua.

Hayo yamesemwa leo Agosti 10, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba katika ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo mkoani humo.

Chongolo ameanza ziara ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho kupitia miradi ya maendeleo, kukagua uhai wa chama na kuhamasisha wananchi kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanywa Agosti 23,mwaka huu.

Akiwa Bumbuli,Chongolo alipokea kilio cha wananchi wa Lushoto kuhusu kiwanda hicho na ndipo Mkuu wa Mkoa akatoa taarifa akisema serikali inatambua kilio hicho na imeshachukua hatua na kuwa Septemba mwezi ujao kiwanda hicho kitaanza majaribio ya kuchakata chai kwa miezi mitatu.

"Hatua zimeshachukuliwa na serikali kukifufua na mwezi ujao Septemba majaribio ya kuchakata chai yanaanza kwa miezi mitatu na Desemba kitafunguliwa,"amesema Mgumba.

Akizungumzia kiwanda hicho,Chongolo amesema dhamira ya serikali ni kuona kiwanda hicho kinafanya kazi ili wananchi wapate ajira na wakulima wa chai wauze malighafi yao na kujipatia kipato na kusema kiwanda hicho ni lazima kianze kazi.

"Lengo la serikali ni kuhakikisha kiwanda hicho kinafufuliwa na kuanza kazi wananchi wapate ajira lakini wakulima wauze chai yao na sio kuharibikia shambani,"amesema Chongolo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live