Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha bidhaa za ngozi chatakiwa kuongeza uzalishaji

Ngoziiiii.jpeg Kiwanda cha bidhaa za ngozi chatakiwa kuongeza uzalishaji

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amekitaka kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro kuongeza uzalishaji wa bidhaa, ili ziweze kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo mkoani Kilimanjaro, kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kutatua changamoto zilipo kiwandani hapo.

Aidha, amesema bidhaa hizo kama viatu, mabegi na pochi zinazotengenezwa na Kiwanda hicho kwa kutumia malighafi za ndani ya nchi zina asilimia 100 ya kukidhi vigezo vya kuingia katika soko la Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live