Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha betri kujengwa nchini

Byabato Kiwanda cha betri kujengwa nchini

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TANZANIA kwa kushirikiana na serikali ya Marekani inakamilisha taratibu za ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini ya kutengenezea betri za magari ya umeme kinachotarajiwa kukamilika mwaka 2026.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Afrika Mashariki Stephen Byabato ameyasema hayo leo Novemba 8, 2023 akijibu swali Bungeni lililoulizwa na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Ameir Abdallah Ameir aliyetaka kujua mchango wa diplomasia ya uchumi katika kuleta mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia na sekta za uzalishaji.

Amesema Diplomasia ya uchumi ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayojumuisha mipango na mikakati ili kunufaisha taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa unaofanyika kupitia ushirikiano baina ya Tanzania, mataifa mbalimbali, jumuiya za kikanda na za kimataifa.

Pia, ujenzi wa kiwanda hicho kitaleta teknolojia mpya ya utengenezaji wa vifaa vya magari, kuhaulisha teknolojia nchini na kuibua vipaji vipya kwa vijana watakaopata ajira katika Kiwanda hicho.

Amesema diplomasia ya uchumi inasaidia upatikanaji wa masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi.

“Mwezi Septemba, 2023 Tanzania imeuza tani 13,708 za nyama ikilinganishwa na tani 1,777 zilizouzwa mwaka 2020/21,” amesema Byabato na kuongeza

“Masoko hayo yamepatikana katika nchi za China, Kuwait, Oman, Qatar, Vietnam na Umoja wa Falme za Kiarabu….; “masoko haya yamechochea sekta ya uzalishaji kwa ujumla wake,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live