Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda cha Mkulazi chatakiwa kuanza kazi mara moja

Pindi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Dkt. Pindi Chana akipokea

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imehimiza mkandarasi anayesimamamia kazi ya ujenzi Kiwanda cha Sukari Mkulazi kufanya kazi hiyo ndani ya muda ulioweka kwenye Mkataba.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Balozi Dkt. Pindi Chana alipotembelea kiwanda cha hicho kwa lengo la kujionea maendeleo na hatua ya ujenzi zilipofikiwa katika kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Ameelekeza Bodi ya Kiwanda pamoja na Wataalamu kuweka bima kwa ajili ya Kiwanda cha Sukari Mkulazi.

"Tunahitaji kuendeleza ushirikishwaji wa ujenzi wa kiwanda kwa sababu wananchi waliozunguka eneo la ujenzi wa kiwanda wanamatumaini makubwa," alisema Balozi Chana.

Amefafanua kwamba Kiwanda cha Sukari Mkulazi kikianza kazi kitapunguza tatizo kubwa la uhitaji wa sukari nchini na tunapaswa kuzalisha sukari nyingi ya kutosha ili tuweze kusafirsha nje ya Nchi.

"Ni lazima turatibu kwa pamoja ili kiwanda hiki cha sukari kianze kufanya kazi mwezi wa nane," alisisitiza Balozi

Aidha alimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ujenzi wa kiwanda hicho.

"Ipo tija ya uwepo wa kiwanda hiki na Kuna Political will ipo hivyo bodi na wataalamu kujipanga kuona ujenzi unakamilka kwa wakati,” alisisitiza

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cha sukari Mkulazi Dkt. Hildelitha Msita amesema mradi huu ni mradi mkubwa na una matarajio makubwa kwa Taifa, tutasimamia mradi huu kwa mujibu wa muda wa mkataba uliowekwa na hakutakuwa mabadiliko ya muda.

Awali akitoa taarifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkulazi Bw. Selestine Some amesema maeneo mbalimbali ya ujenzi wa kiwanda yapo katika hatua ya msingi na wameanza kupandisha vyuma kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya kiwanda ambayo itaenda pamoja na kufunga baadhi ya mitambo ya kiwanda.

"Mpaka sasa tumepokea kontena 63 za vifaa vya viwanda na tunatarajia kupokea kontena 450 kwa supplier wa mitambo ya kiwanda," alieleza Selestine

Kwa upande Mkandarasi Msaidizi John Bura amesema ujenzi wa kwanda hicho amesema wanashirikiana na Mkandarasi Mkuu kumaliza mradi kwa wakati kwa kuhakikisha tunaongeza nguvu kazi kwa kuongeza rasilimali watu na kazi inafanyika masaa 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live