Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kituo cha gesi Dar kukamilika Desemba

Finland Yachunguza Kuvuja Kwa Bomba La Gesi Asilia Kituo cha gesi Dar kukamilika Desemba

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujenzi wa Kituo cha Kushindilia na Kujaza gesi asilia (CNG) kilichopo Barabara ya Sam Nujoma mkoani Dar es Salaam umefikia asilimia 33.5.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Balozi Ombeni Sefue amesema kutokana na kasi iliyopo sasa ya utekelezaji mradi huo, kituo hicho kitakamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Amesema kituo hicho ni kituo mama cha kujaza na kusambaza gesi katika mikoa mbalimbali kwa kuanza na mikoa ya Dodoma na Morogoro pia kusambaza gesi katika vituo vingine vidogo vitakavyojengwa katika maeneo ya Muhimbili na Kibaha mkoani Pwani.

Balozi Sefue amesema uundaji wa mitambo itakayokuja kusimikwa katika mradi huo unaendelea nchini China na umefikia asilimia 76.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live