Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitila: Tunazingatia vigezo maalum kumpokea muwekezaji

Profesa Kitila Mkumbo.jpeg Kitila: Tunazingatia vigezo maalum kumpokea muwekezaji

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kutokana na Tanzania kuwa na fursa mbalimbali za uwekezaji serikali inazingatia vigezo maalum ili kuweza kutambua aina gani ya mwekezaji anayepaswa kupokelewa nchini.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma Waziri Prof. Mkumbo amesema serikali inahakikisha inapokea uwekezaji ambao utakidhi mahitaji ya bidhaa za ndani, aina ya uwekezaji unaoweza kuongeza thamani katika bidhaa au mazao pamoja na kusaidia kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi ili kuongeza fedha za kigeni.

Prof. Mkumbo ameongeza kuwa serikali lazima ijiridhishe kuwa uwekezaji unaotaka kufanyika nchini utasaidia kuzalisha ajira kwa Watanzania, pamoja na kuzingatia uwekezaji ambao utazalisha utajiri kwa Watanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live