Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiteto wanunua petroli kwa Sh 5,000 kwa lita

Waagizaji Mafuta Wakanusha Upotoshaji Unaosambazwa Mitandaoni.jpeg Kiteto wanunua petroli kwa Sh 5,000 kwa lita

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uhaba wa mafuta uliodaiwa kujitokeza maeneo mengi hapa nchini umetajwa kuathiri wananchi wengi hasa maeneo ya vijijini wilayani Kiteto.

Wakizungunza na Mwananchi Digital baadhi ya wananchi leo Alhamisi Julai 3, 2023 wamesema kwa sasa wanaathirika kwa kukosekana mafuta hayo kwenye vituo vya mafuta.

"Biashara ya mafuta ya petroli inafanywa na madereva wa bodaboda ambao wao wanaenda wilaya za jirani ambazo ni Kongwa na Chemba mkoani Dodoma kuchukua nishati hiyo na kuja kuuza huku Kiteto," amesema Mussa Jamal ambaye ni mkazi wa eneo hilo.

Amesema hakuna kituo cha mafuta Kibaya kinachouza sasa mafuta aina ya petroli kati ya vituo vinne vilivyopo mjini Kibaya Kiteto hivyo wanaosaidia kupatikana nishati hiyo ni bodaboda ambao wanauza bei ya juu.

"Mafuta tunatoa eneo la Mjiro iliyopo wilaya ya Chemba km 49 na awali tulitoa Dabalo iliyopo wilaya ya Kongwa na kuja kuuza hapa kiteto kwa lita moja Shilingi elfu 5,000," amesema Hamisi Abrahamani dereva boda Kibaya.

"Pamoja na kazi ya boda ninayofanya ila kuuza mafuta ya vibobo inanipa faida kubwa sana. Napata faida mara mbili natamani kuacha sina hata haja ya kupiga tripu ya boda tena," amesema Abrahamani.

Nao baadhi ya wananchi wa mji wa Kibaya wamesema wanashindwa kufanya shughuli zao kwa wakati kutokana na kupanda kwa gharama hiyo ya mafuta ya petrol.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live