Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitaraka kuzalisha mifugo kibiashara

Ulega Pic Data Kitaraka kuzalisha mifugo kibiashara

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (Mb) amesema kuwa Serikali imedhamiria kulitumia eneo la kupumzishia mifugo la Kitaraka lililopo wilayani Manyoni, Singida liweze kutumiwa na vijana watakaohitimu mafunzo katika vituo atamizi kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji wa mifugo kibiashara ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Ulega alibainisha hayo wakati wa kikao baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba alipokutana nae katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida jana Januari 30, 2023.

Wakati wa mazungumzo yao, Ulega alimueleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa lengo la ziara yake ni kujadiliana nae kuhusu dhamira ya Serikali ya kutaka kulitumia eneo la Kitaraka kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji wa mifugo ili kuwawezesha vijana kujipatia ajira lakini pia kuzalisha malighafi ya uhakika kwa ajili ya viwanda vya nyama na kuifanya sekta ya mifugo kuchangia ipasavyo katika pato la taifa na la mtu mmoja mmoja.

Alisema kuwa kupitia programu ya vituo atamizi iliyoanzishwa na Serikali kwa ajili ya kuwafundisha vijana ufugaji wa kisasa, Serikali imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufuga kibiashara kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live