Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiswahili kutumika uchumi wa kidigitali

Uchumi Kupanda Kiswahili kutumika uchumi wa kidigitali

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa washiriki wa Kongamano la Lugha za Asili kujielekeza katika kupanga mikakati itakayohakikisha Kiswahili na lugha nyingine za asili zinapata fursa katika uchumi wa kidijiti.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza diplomasia ya kiuchumi na kiutamaduni lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Points by Sheraton, Jijini Dar es salaam.

Amesema kongamano hilo linapaswa kuangazia namna ambavyo Kiswahili pamoja na lugha nyingine za asili za Afrika zitakavyotumika kuendeleza teknolojia za asili, kuchochea uvumbuzi, uwekezaji na kukua kwa diplomasia.

Aidha Dkt. Mpango amesema Kongamano hilo linapaswa kusaidia kuonesha fursa zilizopo katika matumizi ya lugha za asili ili kuwafanya vijana kujipatia stadi na maarifa mbalimbali katika kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kiteknolojia ndani na nje ya bara la Afrika.

Amesema kupitishwa kwa Kiswahili kuwa lugha rasmi katika Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kumepanua wigo wa matumizi ya lugha hiyo na kuleta fursa mbalimbali za kiuchumi na kiutamaduni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live