Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

King ahoji fedha za miamala ya mitandao

Tozo Ed King ahoji fedha za miamala ya mitandao

Mon, 9 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jangombe (CCM), Ali Hassan Omar King amehoji ni lini Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) itasitisha kukusanya na kuzirudisha fedha za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) zilizokwisha kusanywa kutoka kwenye miamala ya mitandao ya simu iliyofanywa Zanzibar.

Akiuliza swali hilo leo Jumatatu Mei 9 2022, King amesema hilo linatokana na kiasi kilichokusanywa ni asilimia 18 lakini fedha zilizowasilishwa Mamlaka ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) ni asilimia 15 ya kiwango cha fedha ya makato hayo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema sheria za VAT kwa pande zote za Muungano zimeweka msingi wa kutoza na kukusanya VAT pale ambapo huduma inapotolewa.

Amesema huduma ikitolewa Tanzania Bara, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoza VAT ya asilimia 18 kwa mujibu wa Sheria ya VAT inayotumika Tanzania Bara.

Amesema huduma ikitolewa Zanzibar, Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) inatoza VAT ya asilimia 15 kwa mujibu wa sheria ya VAT inayotumika Zanzibar.

Amesema ili kutambua sehemu ambapo huduma imetumika, Serikali za pande mbili za Muungano ziliunda mfumo wa kielektroniki ujulikanaokama ‘Electronic Revenue Collection System (e-RCS)’ wenye uwezo wa kutambua miamala yote inavyofanyika na hivyo kusaidia kutunza takwimu sahihi zamauzoyanayotokana na miamala ya mitandao inayofanywa na watumiaji wa kila upande.

Advertisement Amesema mfumo huu unasimamiwa na kamati ya wataalamu wa kodi kutoka MamlakayaMapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

“Mifumo ya kampuni zote za simu hapanchini imeunganishwa na mfumo wa Serikali wa e-RCS na taarifa za miamala ya mitandao hutolewa kila mwezi ikiainisha bayana huduma zilizotumika Tanzania Bara na zile zilizotumika Zanzibar,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live