Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana aeleza Serikali itakavyotatua changamoto bei pamba

Spika Tulia, Kinana Watoa Ya Moyoni Bwawa La Mwalimu Nyerere.jpeg Kinana aeleza Serikali itakavyotatua changamoto bei pamba

Sun, 30 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amewaeleza wananchi wa Itilima jinsi serikali itakavyotatua changamoto ya bei ndogo ya pamba nchini na uvamizi wa tembo katika makazi ya wananchi.

Kinana ametoa kauli hiyo jana Julai 28, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Laini A wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu akiwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, uhai wa Chama na kusikiliza changamoto za wananchi.

Akiwa mkoani humo Kinana alipokea malalamiko ya wananchi hasusan wakulima wa pamba kwamba wanatumia gharama kubwa kulima zao hilo, lakini changamoto inayowakabili ni bei ndogo, hivyo walimuomba awasaidie kufikisha kilio chao kwa Chama na serikali upatikane ufumbuzi wa bei ya pamba.

Kinana baada ya kuwasikiliza wakulima hao aliowapa nafasi ya kuuliza maswali, alisisitiza kwamba kuondoa changamoto ya bei ndogo ya pamba, serikali kuu ijitahidi kutengeneza viwanda vya kutengeneza nyuzi, kuchakata pambana na kutengeneza nguo kusiwe na ulazima wa kupeleka pamba nje ya nchi.

Miongoni mwa changamoto hizo, ni pamoja na Bei ndogo ya pamba, upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo na uvamizi wa tembo katika makazi na maeneo ya shughuli za binadamu.

Akijibu changamoto hizo alisisitiza kuwa amechukua changamoto hizo na atakwenda kuzungumza na viongozi wanaohusika.

Hata hivyo Kinana alisema baadhi ya hatua ambazo zitasaidia kukabiliqna na changamoto katika zao la pamba ni muhimu kujenga viwanda vya nyuzi na nguo.

Pia, Kinana alisema ni muhimu kila mkulima ahakikishe analima kisasa, akitoa mfano mkoani Singida alisema kuna mkulima wa pamba anayelima kisasa katika heka moja anapata kilo 1,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live