Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Killango amtaka Magufuli kuwekeza nguvu zao la pamba

50538 KIL

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa kuteuliwa (CCM), Anne Killango Malecela amemtaka Rais John Magufuli kuwekeza nguvu katika zao la pamba ili kuinua uchumi wa nchi.

Killango ametoa kauli hiyo bungeni leo Alhamisi Aprili 4, 2019  akichangia hotuba ya bajeti iliyowasilishwa mapema leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mbunge huyo amesema pamba itapewa kipaumbele, Tanzania inaweza kupiga hatua kubwa ukilinganisha na mataifa mengine.

Amesema Tanzania inashika nafasi ya nane Afrika na 22 ulimwenguni kwa nchi zinazolima pamba, lakini mchango wa zao hilo hauthaminiwi.

"Rais amemteua waziri wa uwekezaji (Angelllah Kairuki), naomba sana waziri nenda ukamsaidie Rais katika zao la pamba, haiwezekani tukashindwa na nchi zinazolima kwa uchache," amesema Killango.

Naye mbunge wa Kijitoupele, Shamsi Vuai Nahodha amesema taifa lenye maono ni lile linalowekeza katika kilimo.

Nahodha amesema huu ni wakati wa Serikali kugeukia kilimo kwani inatabiriwa kuwa miaka ijayo ulimwengu utakuwa na njaa kubwa hivyo ni vyema taifa likajiandaa.

Amesema Watanzania wakijinyima na kuwekeza katika kilimo hawatajuta katika maisha yao badala yake watafurahi.



Chanzo: mwananchi.co.tz