Wizara ya Kilimo imetakiwa kufikiria mawazo mapya kwa ajili ya mipango itakayotoa majawabu ya upatikanaji wa soko la uhakika kwa wazalishaji wa zabibu, hasa uuzaji wa zao la mwisho ambalo ni mvinyo.
Wito huo umetolewa mkoani Dodoma.na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo baada ya kukagua mradi wa Umoja wa Wakulima wa Zabibu wa Ichimada uliopo eneo la Chinangali wilayani Chamwino.
"Nimewasikia hapa mkizungumzia mipango na mambo mengine makubwa, niseme tu nilazima tuache kufikiria mnunuzi wa zabibu yetu kutoka nje ya hapa lazima mtazamo uwepo kwa uzalishaji wa zabibu ya mwisho hapa ambayo tukii-brand inaenda kuwa na jina Dunia nzima. Wenzetu ndiyo wanachofanya, ukifikiria wine tunayoagiza na kuingiza nchini ndiyo inakupa sura ya kiwango matumizi ya wine ndani ya nchi yetu". Amesema Chongolo ambaye anaendelea na ziara yake mkoani Dodoma