Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilimo chatajwa nguzo kuu uchumi wa viwanda

20891 Kilimo+pic TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kilimo kimetajwa kuwa nguzo kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 4, 2018 na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Lindam Group, Zuhura Muro katika mjadala wa Jukwaa la Fikra la Mwananchi unaoendelea muda huu katika ukumbi wa Kisenga jijini Dar es Salaam.

Katika mjadala huo unaorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV,  Muro amesema haiwezekani kuzungumzia viwanda bila kukitaja kilimo.

“Lazima kilimo kipewe kipaumbele kwanza ili kukuza viwanda nchini," amesema.

Amesema lazima kuweka nguvu kwenye uvuvi na ufugaji katika harakati za kukuza sekta ya viwanda nchini.

Mwanafuzni wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Freddy Odo amesema sera ya viwanda haikuanza leo na inatakiwa kuwekewa mkazo ili kufikia malengo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz