Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilimo Tanzania kuchangia Pato la taifa kwa 10%

Kilimo Tanzania 1140x640.jpeg Kilimo Tanzania kuchangia Pato la taifa kwa 10%

Mon, 4 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema Serikali ya Tanzania ina mopango wa kuwainua wakulima na kukiinua kilimo cha Tanzania ili kufikia lengo la kukuza sekta ya Kilimo kwa 10% ambayo imepewa jina la 10/30.

Bashe amesema hayo katika mjadala wa patoja uliowahusisha wadau wa Kilimo uliofanywa na Kituo cha televisen cha Clouds jijini Dodoma Leo Mariam ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugavi wa Kilimo wa Tanzania.

Amesema Inapozungumziwa Ajenda 10/30 ni lengo ambalo wizara ya kilimo imejiwekea kulifikia mwaka 2030, ambapo kwa sasa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano unaisha mwaka 2025 unaeleza kwamba sekta ya kilimo inatakiwa ikuwe kwa wastani wa 5.7% ikiwa ndio marengo yaliyowekwa kwa Miaka mitano.

“Kwa sasa hivi population yetu ni watu Mil 60. Tunatarajia kufika mwaka 2030 itaongezeka kukaribia watu Mil. 80. Unapokuwa na watu 28% wapo kwenye dimbwi la umaskini na uchumi wetu ulivyokaa 61% ya Watanzania wote wapo kwenye sekta ya kilimo ambayo inachangia 26% tu ya pato la Taifa maana yake waliopo mashambani ni 61% ya nguvu kazi ya Taifa,” amesema Bashe.

“Na wanaoshughulika na shughuli za mashambani na uzalishaji ni wastani wa 15%- 20%, Sisi kama wizara tumejiwekea malengo kwamba ifikapo 2030 sekta hii ikue kwa 10% tunaita agenda 10/30.” aliongeza.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Benki ya maendeleo ya Kilimo TADB-Frank Nyabundege, amesema Benki yake inahakikisha inawafikia wakulima wengi zaidi, kwa kutoa msaada kwenye miradi mikubwa ambayo italeta tija katika nchi ya Tanzania na kuhakikisha nchi inafaidika na Kilimo.

“Tunaposema watu zaidi ya 60% katika nchi yetu wapo katika sekta ya Kilimo na kwa nini sekta ya Kilimo inachangia 20% ya pato la taifa.? Tunataka pato la taifa lichangiwe hadi 50% au 60% na Kilimo kwa sababu kama watu wengi wanajishughulisha na Kilimo wanatakiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa,” amesema Nyabundege.

Amesema Benki ya maendeleo ya Kilimo ni benki ambayo kazi zake ni kutekeleza sera ambazo zinawekwa na nchi, na agenda ya 10/30 ni maagizo ambayo yanatakiwa kutekelezwa kwa kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha kibiashara.

Hii Leo maafisa ugani wa Kilimo wa Tanzania nzima wanatarajiwa kugawiwa vitendea kazi katika zoezi ambalo limefanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma katika kufikia lengo la Ajenda 10/30 na Mieni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Vitendea kazi hivyo kwa Maafisa Ugani nchini ni p[amoja na pikipiki 2,000, vifaa vya kupima afya ya udongo (soil agro scanner) 143, simu janja 384 na visanduku yva ufundi vya Maafisa Ugani 3,400.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live