Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilimanjaro wapigwa ‘stop’ lumbesa

Lumbesa Kilimanjaro Kilimanjaro wapigwa ‘stop’ lumbesa

Sun, 22 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hayo yamebainishwa na meneja wakala wa vipimo (WMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Masinde wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kuhusiana na operesheni za ukaguzi wa mizani unaoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

"Kwa wafanyabiashara aidha shambani, sokoni au anasafirisha mazao, akibainika amefanya kosa la kufungasha mzigo kwa lumbesa na kuzidisha uzito, adhabu ni kutozwa faini kiasi kisichopungua 100,000 na kisichozidi Sh20 milioni kwa kila kosa moja, kama itakuwa kosa hilo ni kwa mara ya pili analifanya, atatozwa faini isiyopungua Sh500,000 na isiyozidi Sh50 milioni au kupelekwa mahakamani"amesema

Amesema kuwa wameendelea na operesheni za uhakiki wa mizani na vipimo mbalimbali katika masoko na maeneo mengine mkoani humo ili kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafuata sheria, na kwamba hawatamvumilia mfanyabiashara, ambaye atakiuka sheria na kuzidisha uzito kwa kufungasha mazao kwa mtindo wa lumbesa, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwaibia wakulima.

Amesema Mwezi Januari hadi Machi 31 mwaka huu, vipimo 12, 976 vilihakikiwa katika Wilaya ya Moshi ambapo vipimo 2,715 vilikutwa na kasoro na kuagiza virekebishwe.

"Kwa mwezi wa Aprili katika eneo hilo la Wilaya ya Moshi, vipimo 2,023 vilihakikiwa na kati ya hivyo vipimo 540 vilikutwa na kasoro ambapo vilirekibishwa lakini vipimo sita vilikuwa havifai kurekebishwa hivyo vikaondolewa kwenye biashara".

Advertisement Akizungumzia upimaji wa gesi, Masinde amewataka wauzaji wa gesi za majumbani kuhakikisha wanakuwa na mizani na kwamba kwa ambao hawatakuwa nazo, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Masinde amesema pia wamefanya ukaguzi katika maeneo ya biashara za gesi za manyumbani na changamoto kubwa waliyoibaini ni kukosekana kwa mizani licha ya kwamba sheria inaelekeza kuwa na mizani.

Aidha Masinde ametoa wito kwa wananchi, kuhakikisha wanapokwenda kununua mitungi ya gesi, wanapimiwa na kuona kama kiasi kilichoandikwa juu ya mtungi, kinalingana na kiasi kilichopatikana baada ya kupima.

"Tumekuwa tukitoa pia elimu kwa wananchi, ili kufahamu ni vitu gani vya kuzingatia wanapokwenda kununua gesi, na niwasihi wananchi mkoani hapa, wahakikishe wanapokwenda kwenye maduka kununua gesi mtungi unapimwa ili ajiridhishe na kile anachonunua, na titapita mtaa kwa mtaa, kijiji jwa kijiji, kufanya ukaguzi wa mizani, ili kumlinda mlaji" amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live