Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikao utekelezaji miradi ya nishati ya kupikia

Gesi Urahis Serikali Kikao utekelezaji miradi ya nishati ya kupikia

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tine Tonnes.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam viongozi hao wamejadili kuhusu utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia.

Dk. Jafo amemueleza, Balozi Tinnes dhamira ya serikali katika kuimarisha upatikanaji wa nishati safi na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kwa kuanza na taasisi zenye kulisha idadi kubwa ya watu. - Amesema Serikali inaendelea kuwekeza na kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan ya gesi katika shule na vyuo mbalimbali ili ziachane na matumizi ya kuni na mkaa ambayo inaonekana kuwa ni ya gharama zaidi. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live