Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na Naibu wake Alexander Mnyeti wamepanga kuongeza kasi ya kuongeza tija kwenye ufugaji na uvuvi hapa nchini.
Viongozi hao wamejadili namna ya kuhusisha vijana kwenye mradi wa BBT katika sekta zote mbili kama ambavyo wameagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Waziri Ulega amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye sekta ya mifugo na uvuvi utafanikiwa ikiwa viongozi wote kwenye wizara watatimiza wajibu wao.
Mbali na mradi wa BBT wizara hiyo pia inatekeleza mradi wa uvuvi kwenye maziwa na bahari kuu na hivi karibuni wametoa boti za uvuvi kwa wavuvi wilayani Kilwa mkoani Lindi.