Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijani Bond yakusanya Sh171 bilioni

FEDHA Kijani Bond yakusanya Sh171 bilioni

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna wa Uendelezaji wa sekta ya Fedha kutoka wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamaja ameipongeza Benki ya CRDB kwa kukusanya shilingi Bilioni 171 kupitia Hati Fungani yake ya Kijani ambayo itasaidia kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutoa ajira kwa vijana na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Dkt. Mwanjala amesema makusanyo hayo ni sawa na faida ya shilingi Bilioni 171.82 sawa na asilimia 429.55 ikilinganishwa na lengo la kupata shilingi Bilioni 40 zilizopangwa hapo awali.

Mbali na faida hiyo, Hati Fungani hiyo pia imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemas Mkama, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Mary Miniwasa wamesema hayo ni mafanikio makubwa katika masoko ya mitaji nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameeleza kuwa asilimia 99 ya uwekezaji wa Kijani Bond unatokana na wawekezaji wa ndani, huku shilingi Bilioni 140 zikiwa ni fedha mpya katika mzunguuko, jambo ambalo litachochea kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live