Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea mradi wa Kimkakati wa kilimo cha Miwa na uzalishaji wa sukari unatekelezwa na kampuni ya Bagamoyo Sugar Limited ili kukagua utekelezaji wa mradi huo.
Tumekuja kukagua maendeleo ya mradi huu kujua kama unachangamoto zozote tuweze kuzitatua alisema Dkt. Kijaji. Mradi huo ambao unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kwa sasa umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake.
Ushuhuda kuwa mpango Mkakati wa Taifa wa kuhakikisha Agenda ya Tanzania ya Viwanda vya kimkakati ili kutosheleza mahitaji ya bidhaa muhimu hapa nchini unafanikiwa kwa kushirikiana na Sekta binafsi.
Tunatarajia kurudi hapa tarehe tano mwezi wa saba kwani tumeahidiwa mradi utakuwa umeanza uzalishaji kama walivyotuahidi.
Ajira za moja kwa moja.
Kampuni hii itakapokuwa imekamilisha uwekezaji wake tunatarajia kuwepo kwa jumla ya ajira za moja kwa moja zaidi ya 1500 za na zisizokuwa za moja kwa moja ni 3000.
Thamani ya Mradi na manufaa Ya Mradi kwa Watanzania Kampuni hii inatarajia kuwekeza jumla ya Dola za Kimarekani zipatazo Milioni 193.75 ambazo zitawekezwa katika kilimo cha miwa, miundombinu ya umwagiliaji, ujenzi wa kiwanda, ununuzi wa mitambo, na vifaa mbalimbali vinavyohitajika..
Mahitaji ya Sukari na uzalishaji Mahitaji ni kati ya tani 550,000-600,000 kwa mwaka na inatarajiwa kupanda hadi kufikia tani 800,000. Kiasi kinachozalishwa kwa sasa ni takribani tani 300,000.
Mradi huu unatarajiwa kuzalisha tani 30000 utakapoanza na utakapokamilika phase zote tatu utazalisha tani laki moja (100,000) za sukari kwa mwaka.
Serikali inafanya maboresho mbalimbali ili kuboresha mifumo na kurahisisha utoaji wa huduma zote za vibali na usajiri kwa wawekezaji.
Lengo ni kuhakikisha kuwa tunakabiliana na changamoto zote za wawekezaji na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja kwa haraka ili wawekezaji waweze kuwekeza miradi yao waliokusudia katika kipindi husika bila kukwamishwa na huduma za Taasisi zetu.