Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijaji: Royal Tour imejaza hoteli Dar, Arusha, Kilimanjaro

KIJAJI WEB 1 Ashatu Kijaji, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kwamba hoteli katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro zimejaa kutokana na matokeo chanya ya filamu ya Royal Tour aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hasan ya kuhamasisha utalii.

Hayo ameyasema katika maonyesho ya 9 ya biashara na utalii yanayofanyika jijini Tanga na kusema kuwa filamu ya The Royal Tour imeleta ushawishi kwa wawekezaji na watalii kuja nchini ambapo amewataka wafanyabiashara kujenga hoteli za kisasa na kutoa huduma zinazohitajika. 

"Hoteli zote zimejaa kwa miezi mitatu ijayo hivyo nimewaambia umoja wa mahoteli hapa Tanga, mnaposikia majirani zenu wote hawana nafasi ya kuhudumia kilichobaki mbele yako ni wewe kujipanga vizuri na sasa ni Jiji la Tanga na mahoteli yake kupokea watalii na wawekezaji, "amesema Waziri Dkt. Kijaji.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live